CRM LAND CONSULT (T) LTD YAONGOZA UPANGAJI MIJI TANZANIA: Yapokelewa kwa vifijo na ndelemo wilayani Gairo
PROGRAMU
YA KUPANGA, KUPIMA NA KUMILIKISHA ARDHI GAIRO MJINI
IMEANDALIWA
NA KUWASILISHWA
NA
ISMAIL
R. CHINGWELE
MTAALAM
MSHAURI WA MIPANGO MIJI NA ARDHI
CRM
LAND CONSULT (T) LTD
DAR ES
SALAAM-TANZANIA
1.0 Utangulizi
Tanzania
inakabiliwa na ongezeko kubwa la watu na mahitaji ya ardhi kwa matumizi
mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Ukuaji
wa kasi wa miji usiozingatia mpangilio wa mipango miji pamoja na kuongezeka kwa
kasi kwa ujenzi holela kumesababisha kuwa na makazi yasiyo na huduma muhimu za
kijamii pamoja na miundombinu na mazingira yasiyo safi na salama kiafya,
ambayo, pamoja na mambo mengine, husababisha magonjwa ya milipuko. Pia ujenzi
holela huikosesha Serikali mapato yatokanayo na kodi za ardhi.
Aidha,
kutokuwepo kwa mpango wa matumizi ya ardhi katika maeneo ya vijijini, hususan
yanayotenganisha maeneo ya malisho ya mifugo na kilimo, uvamizi na uanzishwaji
holela wa mashamba, ni chanzo cha muingiliano wa matumizi ya ardhi baina ya
wakulima na wafugaji. Hali kama hii hutokea pia kati ya wakulima na wawekezaji,
Serikali za Vijiji na Hifadhi za Taifa, vijiji na vijiji na wilaya na wilaya.
Hali hii husababisha uvunjifu wa amani na hata kusababisha baadhi ya watu
kupoteza maisha na mali zao.
Vilevile,
kutofautiana kwa mipaka ya kiutawala inayotokana na Matangazo ya Serikali (GN),
ramani za upimaji wa vijiji na ramani za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012
kumechangia kuwepo kwa mpaka zaidi ya mmoja na hivyo kusababisha migogoro ya
mipaka katika maeneo husika.
Sera
ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995, inabainisha haki ya kila Mtanzania kumiliki
ardhi nchini. Utekelezaji wa Sera hii unafanyika kwa kutumia Sheria ya Ardhi
Na. 4 ya Mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya Mwaka 1999. Sheria
nyingine ni Sheria ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Na. 2 ya Mwaka 2002, Sheria
Na. 6 ya Matumizi ya Ardhi ya Mwaka 2008 na Sheria Na. 8 ya Mipango Miji ya
mwaka 2007.
Utekelezaji
wa Sera na Sheria, pamoja na mambo mengine, unalenga kuhakikisha kwamba, elimu
kuhusiana na Sheria hizi inatolewa na kuwafikia wananchi; mipaka ya Vijiji
inapimwa; Vijiji vinaandaliwa Mipango ya Matumizi ya Ardhi; kila mji
unaandaliwa Mpango wa Jumla unaotoa mwongozo wa ukuaji wa mji; viwanja katika
maeneo mapya vinapimwa na kumilikishwa; maeneo yaliyoendelezwa kiholela
yanarasimishwa na wananchi wanapatiwa hatimiliki zao; kila kipande cha ardhi
kijijini kinapimwa na kumilikishwa; na migogoro ya ardhi baina ya watumiaji
inatatuliwa.
Fursa
zilizopo katika kutekeleza program hii ni pamoja na kuwapo kwa miradi mingine
inayoendelea kutekelezwa inayofanana na progamu hii, utayari wa wananchi
kupimiwa maeneo yao na kusuluhisha migogoro inayowakabili, pamoja na utayari wa
Serikali kushirikiana na sekta binfsi katika utekelezaji wa Programu hii. Fursa
nyingine ni kuwapo kwa wataalam wa kutekeleza kazi hii, utashi wa viongozi wa
kisiasa kwa kushirikiana na Serikali na kuhakikisha wananchi wanapimiwa ardhi
yao na kumaliza migogoro inayowakabili.
Katika
kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya ardhi, hususan migogoro ya
ardhi, Serikali imepanga kutekeleza Programu ya Kitaifa ya Kupanga, Kupima na
Kumilikisha Ardhi, ili kwenda sambamba na mpango elekezi wa Taifa wa muda mrefu
(2016/2017 – 2020/2021) ambapo sekta ya ardhi imepewa kipaumbele. Hata hivyo
serikalin kwa kutambua ufinyu wa bajeti uliopo, iliazimia kushirikisha sekta
binfsi katika utekelezaji wa programu hii.
Madhumuni
ya Program hii ni kuhakikisha kuwa ardhi yote ya Tanzania inapangwa, kupimwa na
kumilikishwa na kumbukumbu zake kuhifadhiwa, ili kuweka mazingira bora ya usimamizi
wa ardhi.
Matokeo
yanayotarajiwa kutokana na utekelezaji wa Programu hii, ni kuwa na mipaka
sahihi katika ngazi zote za kiutawala (Vijiji na vitongoji ndani ya wilaya).
Aidha, ardhi itakuwa imepangwa, na kila kipande cha ardhi kupimwa na
kumilikishwa. Utekelezaji huo utawezesha
kuwa na usalama wa miliki, kuongezeka kwa thamani ya ardhi na maduhuli ya
Serikali, kurahisishwa upatikanaji wa taarifa za ardhi, kuboreshwa kwa
mazingira, kupungua kwa migogoro ya
ardhi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.
1.1
Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi Gairo
Mji wa gairo ni miongoni mwa miji inayo kua kwa kasi
nchini na inakabiliwa na ongezeko kubwa la watu na Ujenzi holela hivyo kua na
uhitaji wa kurasimishwa na kumilikishwa kwa wananchi ili halmashauri iongeze
mapato yake kupitia kodi ya Ardhi na wananchi pia waweze kutanua wigo wa
dhamana kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa kutumia hatimiliki ya Ardhi watakayo
kua nayo.
Maeneo yalio onekana kua na uhitaji mkubwa Zaidi ni yale
ya katikati ya mji yaani CBD ambayo yanakabiliwa na Ujenzi na ongezeko kubwa la
kazi mbalimbali za kiuchumi. maeneo haya yalionesha uhitaji mkubwa sana wa
kupanga kupimwa na kumnilikishwa kwa wanachi na hii imetokana na ukuaji wa kasi
wa kata hizi usiozingatia sheria za kitaalam za mipango miji ikiwemo sheria ya
mipango miji ya mwaka 2007.
1.2
Hasara za makazi holela katika maendeleo ya mji
Moja ya hasara ya kuwepo kwa makazi holela ndani ya
mji ni kusababisha ugumu wa utoaji huduma za jamii kwa wananchi wanao ishi
maeneo hayo zikiwemo maji safi, maji taka, uhifadhi wa taka ngumu, elimu, afya
na barabara, hasara nyinginezo ni pamoja na;-
- Kutengeneza sura mbaya ya mji
- Hatari ya milipuko ya magonjwa kutokana na ukosefu wa mifereji ya kupitishia maji taka na maji ya mvua wakati wa mvua
- Jamii kukosa dhamana ya kujikwamua kiuchumi na hivyo kupelekea ugumu wa maisha na hali ngumu ya kujikwamua na baa la umasikini
- Serikali kukosa mapato yanayoweza kutokana na kodi ya Ardhi na hivyo kupelekea ufinyu wa majeti ya kazi za kimaenddeleo ndani ya mji
- Migogoro ya matumizi ya Ardhi na mipaka ya viwanja baina ya wananchi. Mfano wa migogoro ya matumizi ya Ardhi hutokea pale kunapokua na muingiliano wa nyumba za ibada na makazi, kumbi za starehe na makazi. N.k
1.3
Njia za kutatua tatizo la makazi holela Gairo
Kupitia sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na ile
ya mipango miji namba 8 ya mwaka 2007 inaelekeza namna ya kutatua tatizo la
makazi holela nchini kua ni kurasimisha na kumilikisha maeneo hayo kwa kupanga,
kupima na kutoa hatimiliki za viwanja katika eneo husika, pia kuzingatia kutoa
maneneo ya huduma ndani ya eneo hilo kama vile maeneo ya shule na zahanati.
Lakini pia Urasimishaji wa makazi holela ulianishwa na
kusisitizwa na waziri wa Ardhi nyumba na maenedelo ya makazi mwaka 2016 pale
alipozitaka halmashauri zote nchini kushirikiana na sekta binafsi kurasimisha
makazi holela ndani ya halmashauri zao kwa kutumia mbinu shirikishi.
Kupitia tamko hilo, andiko hili linalenga kuunga mkono
juhudi za serikali za kutaka kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha
Ardhi nchi nzima pia kuunga mkono juhudi za waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo
ya makazi zinazo lenga kutoa hati za kumiliki Ardhi 400,000 kwa mwaka.
Kukamilika kwa miradi ya urasimishaji ndani ya mji wa Gairo
kutakua na faida zifuatazo;-
- Kudhibiti Ukuaji wa maendeleo holela unaoharibu sura ya mji
- Kudhibiti kuongezeka kwa idadi ya migogoro miongoni mwa watumiaji wa ardhi.
- Kuwa na uhakika wa miliki na matumizi ya Ardhi katika eneo husika.
- Kuimarisha soko la ardhi lisilo rasmi linalo fanywa na wananchi ndani ya mji na hivyo kuwainua kiuchumi wananchi wa hali ya chini wanaotegemea Ardhi kama sehemu ya kujikwamua kimaisha.
- Kupunguza hatari ya milipuko ya magonjwa ndani ya maeneo husika kwa kutenga maneneo ya taka na ifereji ya kusafirishia maji taka na maji ya mvua.
- Kuweka utaratibu wa matumzi bora ya rasilimali ardhi kwa kutatua migogoro, hasa ya mipaka ya viwanja.
- Kuimarisha miliki za ardhi na matumizi yake kwa kuainisha thamani ya miliki hizo katika maisha ya kila siku ya mtu mmoja Mmoja na mji kwa ujumla.
- Kuboresha matumizi na hifadhi ya ardhi kulingana na mapendekezo na uwezo wa walengwa.
- Kuboresha hali ya maisha ya watu kuondoa umasikini na utunzaji wa mazingira ndani ya mji.
Hata hivyo faida hizo zimegawanywa katika makundi
manne kama ifuatavyo;-
2.0 Faida za Programu Gairo
Utekelezaji wa Programu ya
kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini unalenga kutatua
changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya ardhi. Kazi hii inahitaji
msukumo na ushirikishwaji wa wadau na jamii nzima unaozingatia misingi ya haki
na demokrasia. Kazi zitakazotekelezwa katika Programu hii ni pamoja na
uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa umma, uhakiki wa michoro iliopo, uandaaji
wa mipango ya matumizi ya ardhi, upimaji na umilikishaji wa kila kipande cha
ardhi.
Utekelezaji wa Programu hii
unatarajiwa kuleta matokeo chanya yatakayoleta faida za kijamii, kiuchumi,
kimazingira na kiutawala kwa mtu mmoja mmoja, Taasisi na Taifa kwa ujumla.
2.1 Faida za Kiuchumi
Utekelezaji wa Programu hii
utaongeza thamani ya ardhi na kuibadilisha kutoka mtaji mfu kuwa mtaji hai na
hivyo kuifanya itoe mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Upimaji na
umilikishwaji wa vipande vya ardhi
Mijini na vijijini utachangia ustawi wa nchi kupitia kodi ya pango la ardhi kwa
wamiliki wa ardhi, kuongeza wigo wa uzalishaji mali kupitia biashara na mikopo
itakayotolewa na vyombo vya fedha.
Hivyo, faida za kiuchumi
zitakazopatikana baada ya Programu hii kutekelezwa ni pamoja na kuongezeka kwa
maduhuli ya Serikali yatokanayo na ardhi; kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji
mali; kuongezeka kwa thamani ya ardhi na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanyia
biashara na shughuli za uwekezaji.
2.2 Faida za Kimazingira
Katika utekelezaji wa Programu
hii, kila kipande cha ardhi kitapangiwa matumizi na kupimwa, hivyo ardhi yote
ya Tanzania itakuwa na matumizi yanayojulikana na kuondoa mwingiliano wa
matumizi. Vilevile, mipango ya matumizi
ya ardhi itasaidia ardhi yote kutunzwa na watumiaji husika na kuhifadhiwa kwa
maliasili zilizopo na mazingira kwa ujumla. Pia, jamii inayozunguka maeneo
yaliyohifadhiwa itawezeshwa kutambua mipaka yao na kuwa na mipango ya matumizi
ya ardhi na kudhibiti uvamizi wa maeneo hayo.
Aidha, utekelezaji wa Programu
hii utajenga uelewa wa jamii wa kutunza ardhi wanayomiliki dhidi ya uharibifu
wowote; kuwezesha kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi;
kuboresha makazi ya wananchi na kuleta usalama na ustawi wa maliasili za Taifa.
2.3 Faida za Kiutawala
Matokeo ya utekelezaji wa
Programu hii ni kuwa na mipaka iliyohakikiwa, kurekebishwa na kuridhiwa na
pande husika. Hali hii itawezesha kuondokana na migogoro ya mipaka na hivyo
kuleta utulivu na amani katika jamii.
Mipaka isiyo na kasoro itawasaidia watawala kufahamu
maeneo ya mamlaka yao kwa usahihi hivyo kuwawezesha kuratibu shughuli za usimamizi
wa mipango mbalimbali. Aidha, itawasaidia wananchi kujua wanakowajibika
kiutendaji na mahali wanapostahili kupata huduma mbalimbali kwa ajili ya
shughuli za kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Kazi ya usimamizi wa shughuli za maendeleo, ulinzi na
usalama hufanyika ndani ya mipaka ya kiutawala inayofahamika hivyo utekelezaji
wa programu hii utawezesha kuwepo na uwajibikaji na ufuatiliaji wa karibu.
Pia vilevile utekelezaji wa program hii utaisaidia
serikali kupata faida za moja kwa moja kama vile kupimiwa maeneo yote ya
taasisi( shule, zahanati, maeneo ya wazi na barabara za ndani) bure na
kukabidhiwa mkurugenzi wa wilaya kwa niaba ya wananchi, kwa kufanya hivyo
itasaidia utambuzi wa maeneo hayo na hivyo kudhibiti uvamizi wa wananchi katika
maeneo hayo.
Kwa upande wa vijijini, baada ya uhamasishaji
kukamilika na wananchi kujenga mwamko wa utekelezaji wa program hii, serikali
pia kupitia halmashauri hii, itapata maeneo mapya kutoka kwa wananchi yatakayo
weza kutumika kwa fidia ya maeneo ya umma
2.4 Faida za Kijamii
Kijamii, utekelezaji wa
Programu utasaidia kutatua migogoro ya ardhi iliyopo baina ya watumiaji, kuzuia
migogoro ya mipaka ya kiutawala, na hivyo kudumisha amani na utulivu katika
jamii, na kuleta maelewano kati ya watumiaji mbalimbali wa ardhi
3.0 Eneo
lililo athiriwa zaid na makazi holela gairo
Wilaya ya Gairo ni miongoni
mwa wilaya zinazokua kwa kasi kubwa kulinganishwa na wilaya nyingine nchini.
Wilaya hii ni miongoni mwa maeneo nchini yanayo kabiliwa na ongezeko kubwa la
watu na shughuri za kiuchumi zinazo pelekea mahitaji ya Ardhi kuongezeka siku
hadi siku. Miongoni mwa maeneo yalio athiriwa zaid wialayani Gairo ni pamoja na
kata Gairo, Luhwaji, Majawanga, Ukwamani, Mkalama, Meshugi na Msingisi zote
hizi zinapatikana ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa Gairo.
Kijografia eneo hili
linaonekana kuania ngazi ya taifa, mkoa, wilaya na mji mdogo kama invyoonekana
katika ramani zifuatazo.
Kielelezo
namba 1: Ramani ya Tanzania kuonesha mkoa wa Morogoro ambao ndani yake
hupatikana wilaya ya gairo

Kielelezo
namba 2: Ramani ya mkoa wa Morogoro kuonesha wilaya ya Gairo ambayo ndani yake
hupatikana mji mdogo wa Gairo

Kielelezo
namba 3: Ramani ya wilaya ya Gairo kuonesha mji mdogo wa Gairo ambayo ndani
yake kuna kata zilizo athirika zaid

Kilelezo namba 4: Ramani ya mji mdogo wa Gairo kuonesha
kata zenye maeneo yaliuo athirika kwa makazi holela

Hata hivyo kutoka kilelezo namba 4, ifuatayo ni picha
ya anga kuonesha hali halisi ya kata ya Gairo ambayo ni miongoni mwa kata saba
zilizo athirika zaid na makazi holela.
Kwa kawaida ardhi haiongezeki, licha ya kwamba
idadi ya watu na shughuli juu ya ardhi zinaongezeka siku hadi siku. Tanzania,
kama nchi nyingine zinazoendelea ina idadi kubwa ya watu inayofikia kiasi cha
milioni 49 kwa maoteo ya mwaka 2017 yanayotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya
mwaka 2012. Kasi ya ongezeko la idadi ya
watu ni asilimia 2.7 kwa mwaka ambalo limesababisha mahitaji ya ardhi kwa
matumizi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kuongezeka.
Ukuaji wa Miji midogo kuwa miji mikubwa na
majiji umesababisha kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa ardhi hususan ardhi
iliyopangwa na kupimwa. Pia, kumekuwepo na ukuaji wa kasi wa miji ambao
hauzingatii mpangilio wa mipango miji na kuongezeka kwa kasi kwa ujenzi holela
wenye makazi yasiyo na huduma muhimu za kijamii pamoja na miundombinu na
mazingira yasiyo safi na salama kiafya.
Katika maeneo ya vijijini, matumizi ya ardhi
yamekuwa hayazingatii mpango wa matumizi ya ardhi, yanayotenganisha sehemu za
malisho ya mifugo na kilimo, uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa na uanzishwaji
holela wa mashamba. Hali hii imesababisha uvunjifu wa amani na baadhi ya watu
kupoteza maisha na mali zao.
Aidha, kutofautiana kwa mipaka ya kiutawala
inayotokana na Matangazo ya Serikali (GN), ramani za upimaji wa vijiji na
ramani za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kumechangia kuwepo kwa mpaka
zaidi ya mmoja na hivyo kusababisha migogoro ya mipaka katika maeneo mbalimbali
nchini.
Programu hii ambayo itahusisha kupanga, kupima
na kumilikisha ardhi vijijini na mijini itasaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana
kwa ardhi wakati wote kwa matumizi ya vizazi vyote na kuondoa migogoro ya ardhi
katika jamii. Aidha, kuwa na ardhi iliyopangwa, kupimwa na kumilikishwa
kunaongeza uhakika wa usalama wa milki, thamani ya ardhi na kuchangia kupunguza
umaskini kwa kutumia kikamilifu fursa za matumizi ya ardhi hiyo kama dhamana ya
mikopo kutoka katika taasisi za kifedha.
Vilevile, kuwa na mipaka sahihi ya kiutawala
kunawezesha watawala kufahamu maeneo ya mamlaka yao kwa usahihi hivyo kuwasaidia
katika kuratibu shughuli za usimamizi wa mipango mbalimbali ya kijamii, kisiasa
na kiuchumi.
Taarifa na takwimu zote zinazohusiana na matokeo ya utekelezaji wa
Programu hii zitaingizwa katika Kanza ya Taifa ya takwimu za ardhi kwa ajili ya
utunzaji wa kumbukumbu za ardhi. Kumbukumbu hizo zitakuwa msaada mkubwa katika
kuainisha na kusimamia maeneo yote yaliyokwishapimwa. Pia, taarifa hizo
zitatumika wakati wa utekelezaji wa programu mbalimbali za Kitaifa zikiwemo
Sensa ya Watu na Makazi, vitambulisho vya makazi, anuani za makazi, masuala ya
ulinzi na usalama wa nchi na programu nyingine zinazotekelezwa na Serikali
katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Hata hivyo kwa kutambua umuhimu wa pogramu hii kampuni ya CRM Land
Consult (T) Ltd imedhamilia kushirikiana na serikali pamoja na wananchi
kukamilisha program hii itakayo kua na faida kwa serikali na wananchi kwa
ujumla.
Kampuni y CRM Land Consult (T) Ltd inalenga kufanya yafuatayo ili
kuhakikisha programu inakua na faida kwa wilaya na viunga vyake;-
·
Kuunganisha
wadau mbalimbali wa maendeleo ndani ya mji ili kuwezesha uungwaji mkono wa
programu hii
·
Kuhamasisha
na kutoa elimu kwa wananchi ili kujenga utayari wa kupangwa,kupimiwa na
kumilikishwa maeneo yao
·
Kupanga na
kutenga matumizi mbalimbali ya Ardhi katika vijiji vilivyo pembezoni mwa mji
kwa kushirikiana na wananchi katika maeneo hayo.
Vile vile
kampuni ya CRM Land Consult (T) Ltd ina nguvu kazi na vifaa vya teknolojia ya
kisasa kuweza kufanya kazi hii kwa uharaka Zaidi na ina rasili mali watu wenye
weredi mkubwa wenye uwezo wa kuhamasisha na kutoa elimu yenye kuzingatia sheria
na sera zote za Ardhi kwa wananchi.
CRM Land
Consult (T) Ltd imefanya kazi nyingi ndani ya nchi kama inavyoonekana katika
wasifu wa kampuni uliombatanishwa na andiko hili (rejea wasifu wa kampuni).
Maoni
Chapisha Maoni